Serikali imetoa siku 30 kwa maofisa elimu wa mikoa na wilaya zote nchini kuhakikisha wamelipa madeni yote yanayohusu uhamisho wa waalimu huku ikipiga marufuku kuanzia sasa kufanyika uhamisho holela kwani kuna zalisha madeni yasiyo na lazima ambayo yanasababisha migogoro isiyoisha kati ya Serikali na watumishi wa kada hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, George Simbachawene wakati akiongea na maofisa wa mikoa na wilaya zote mjini Dodoma, amesema kuwa uhamisho usiokuwa wa lazima ni kukiuka waraka uliotolewa na Serikali wa kutozalisha madeni yasiyokuwa na tija ambayo malipo yake hayajaidhinishwa na Mamlaka yeyote.

Aidha, Simbachawene amesema kuwa sekta ya elimu inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu mkubwa wa madarasa ambapo kwa shule za msingi kuna mahitaji zaidi ya madarasa 127000 na madarasa 10200 kwa shule za sekondari huku akizitaka mamlaka za serikali za mitaa kuendelea na utaratibu wa kuwashirikisha wananchi kuchangia nguvu na fedha kwa ajili ya ujenzi  kwani Serikali peke yake haiwezi.

Hata hivyo, maofisa elimu hao wameeleza changamoto mbalimbali zinazo wakabili katika utendaji kazi wao wa kila siku ikiwemo uhaba wa vitendea kazi ikiwemo uhaba wa magari kwaajili ya kutembelea mashule na ukaguzi, bajeti ndogo ya kuendeshea ofisi pamoja na kuingiliwa katika majukumu yao na baadhi ya viongozi na wanasiasa hali inayochangia waalimu kutotimiza majukumu yao.

Mtu mmoja apigwa risasi na kufa mkoani Singida
Video: JPM atoa angalizo zito kwa viongozi, Chadema wapania bunge la Bajeti