Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Usiwz, Xherdan Shaqiri hatimae amefanikisha azma ya kucheza soka nchini England, baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Stoke City akitokea nchini Italia alipokua akiitumikia klabu ya Inter Milan.

Shaqiri, ametambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili wake huko Britannia Stadium, ambapo usiku wa kuamkia jana alikua akifanyiwa vipimo vya afya.

Shaqiri atakuwa akivaa jezi namba 22, ambayo aliithibitisha wakati akitambulishwa kwa waandishi wa habari.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, amekubali kujiunga na klabu ya Stoke City, baada ya uongozi wa Inter Milan kuafiki dau la paund million 12.

Safari ya Shaqiri, kutoka nchini Italia hadi kuelekea England, ilitokana na kutopendezwa na mazingira ya kimaisha huko mjini Milan nchini Italia, na alifikia hatua ya kuwaeleza viongozi wa klabu ya Inter Milan hali hiyo.

Klabu ya Everton ilikua inatajwa kumuwania Shaqiri, lakini mipango yao imeingia gizani kufuatia Stoke City kufanikisha azma ya kumpeleka Britannia Stadium.

Pedro Ampuuza Meneja Wa FC Barcelona
AY: Wasanii Wa Bongo Tukimbie