Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ambaye ni mwanachama wa Chadema, ameendelea kusifia utendaji wa Rais John Magufuli huku akimvuta kuingia upinzani.

Akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Sumaye ameeleza kuwa ingawa Rais Magufuli anafanya kazi kubwa, hataweza kufanikisha kwa kiwango anachokitarajia kutokana na mfumo wa chama alichomo.

Mwanasiasa huyo amelifia zoezi la kutumbua majipu na kubana matumizi lakini ameeleza kuwa atashindwa kutumbua majipu mengine akiwa ndani ya CCM kwakuwa kuna baadhi ya majipu yameweka mizizi mikuu.

“Kwa utaratibu, hata ungekuwa nani, hicho chama kimetawala kwa miaka yote hiyo, watu unawatumbua na wao wana mizizi. Na kama hawana mizizi, wamewekwa kwenye maeneo hayo labda walikuwa na ulinzi fulani,” alisema Sumaye na kuongeza kuwa kuna majipu mengine yamekaa kwenye moyo hivyo hayawezi kutumbuliwa ndani ya mfumo huo.

Aidha, Sumaye alitahadharisha kuhusu zoezi la utumbuaji majipu linalofanywa na baadhi ya mawaziri akieleza kuwa wengine wanaiga na wanaiga vibaya hivyo alishauri kazi hiyo ingefanywa na Rais pamoja na Waziri Mkuu.

Judo Zanzibar Yatoa Ahadi Ya Kurudi Na Ubingwa
Wasira ageuka Mbogo, ajaribu kumgonga na gari mwandishi, kumpokonya kamera