Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imewasili nchini leo June 7 2017 ikitokea Alexandria Misri ilipokuwa imeweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kucheza mataifa ya Afrika 2019 dhidi ya Lesotho.

Tanzania itaingia uwanjani kwa mara ya kwanza ya kuwania kufuzu michuano hiyo dhidi ya Lesotho Jumamosi ya June 10.

Baada ya kuwasili nchini kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema kuwa timu yake imejipanga vizuri kwa ajili ya kuhakikisha kuwa jumamosi wanafanya vizuri kwani wamefanya maandalizi mazuri wa wachezaji wote wapo sawa.

Amesema kuwa Taifa Stars itafanya mazoezi pia baada ya kurudi na amewahakikishia watanzania kuwa wanayomatumaini ya kufanya vizuri dhidi ya Lesotho, hivyo amewataka watanzania kwenda uwanjani kwa wingi siku ya jumamosi kwa ajili ya kushuhudia ushindi wa timu yao ya Taifa.

Naye mchezaji wa Taifa Stars, Simon Msuva amesema kuwa anawaahidi watanzania ushindi kwani yeye pamoja na wachezaji wote wamajipanga vizuri kwa ushindi dhidi ya mchezo wao utakao chezwa Jumamosi, Juni 10.

Magaidi wa IS washambulia bunge la Iran, watu 12 wauawa
Video: ACT wampongeza JPM, wasema amevunja mwiko siasa Tanzania