Mtoto pekee wa star wa muziki wa pop, Whitney Houston na Bobby Brown, Bobbi Kristina Brown amefariki dunia jana (Julai 26) akiwa na umri wa miaka 22.

Kifo chake kimethibitishwa kupitia tamko rasmi na familia ya Whitney Houston iliyotolewa na muwakilishi wa familia hiyo.
Bobbi Kristina alikutwa akiwa mahututi ndani ya sinki la kuogea (bathtub) katika nyumba yao huko Atlanta Januari 31 mwaka huu na kuwekwa katika mashine maalum za kumsaidia kupumua kwa kipindi chote hadi alipopatwa na mauti.

Kwa mujibu wa ripoti za polisi, Kristina alikutwa na majeraha usoni na mdomoni hali iliyoashiria kuwa alishambuliwa muda mchache kabla ya kukutwa katika eneo hilo.

Sababu ya kifo cha Bobbi Kristina imefanana na ile iliyochukua uhai wa mama yake, Whitney Houston ambaye alikutwa ndani ya sinki la kuogea katika hotel moja huko Baverly Hills, California, Februari 11, 2012.

Bobbi Kristina, baba yake na mama pia walikuwa waathirika wa madawa ya kulevya. Ndoa ya Bobby Brown na Whitney ilivunjika rasmi mwaka 2007.

Kwenye mahojiano yake na na Oprah Winfrey mwaka 2009, Whitney alisema ndoa yao ilivunjika kutokana na kupigana mara kwa mara na kusababishiwa msongo wa mawazo na mumewe huyo.

Bobbi Kristina ndiye aliyekuwa mrithi wa mali zote za mama yake.

Zitto Kabwe: ACT Ina Miiko Ya Maadili Tofauti Na Ukawa
Ni Vita Kati Ya Benitez, Van Gaal Na Ramos