Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka  barani Afrika (CAF ) kilichokutana mwishoni mwa wiki jijini Cairo nchini Misri, kimewateua watanzania saba kuwa wajumbe wa kamati zake mbali mbali kwa kwa kipindi cha miaka miwili 2015-2017.

 Walioteuliwa pamoja na kamati zao katika mabano ni:

 1. Leodeger Tenga- (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa Kamati ya Ushauri na Vyama Wanachama).

 2. Jamal Malinzi – (Mjumbe kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20)

 3. Mwesigwa Selestine – (Mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya Miaka 17).

 4. Richard Sinamtwa -(Mjumbe Kamati ya Rufaa)

 5.Dr Paul Marealle -(Mjumbe Kamati ya Tiba)

 6. Lina Kessy -(Mjumbe ya Soka la Wanawake)

 7. Crescentius Magori-(Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la Ndani)

Shirikisho la soka nchini  – TFF linawapongeza wajumbe wote walioteuliwa kuingia katika kamati mbali mbali na linawatakia kila la kheri wanapoiwakilisha nchi yetu.

TFF.

Tetesi Za Usajili Barani Ulaya
Dk. Slaa Kuongeza Nguvu Chadema, Lowassa Achukua Fomu Kwa Mafuriko