Real Madrid watampa David De Gea mwenye umri wa miaka 24, pauni milioni 24 kama ada ya usajili, iwapo atamalizia mkataba wake ulosalia wa mwaka mmoja Old Trafford, wakati atakapoondoka bure msimu ujao (Daily Mirror)

Manchester City wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 28.5 wa beki wa Valencia Nicolas Otamendi, 27, huku Eliaquim Mangala, 24, akitarajiwa kwenda Spain kwa mkopo (Daily Mail)

Manchester City wataongeza dau lao la pauni milioni 43 kumtaka kiungo wa Wolfsburg, Kevin De Bruyne (Sky Sports)

Tottenham wapo tayari wiki hii kutoa dau la pauni milioni 15 kumtaka mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22, huku beki Joleon Lescott, 33, kiungo Stephane Ssesegnon, 31, Brown Ideye, 26 na Victor Anichebe pia wakiruhusiwa kuondoka (Telegraph)

Dau la pauni milioni 5 kutoka Chelsea kumtaka beki wa Galatasaray Alex Telles limekataliwa (Daily Star)

Everton watamnyatia beki wa Swansea Ashley Williams, 30, iwapo John Stones, 21, atakwenda Chelsea (Daily Star)

Meneja wa Everton Roberto Martinez pia anataka kumsajili mshambuliaji wa Dynamo Kiev Andriy Yarmolenko (Liverpool Echo)

Meneja wa West Ham Slaven Bilic anamtaka kipa wa QPR Robert Green, 35, akitaka kuimarisha makipa wake (Sun)

Newcastle na Everton wanamtaka beki Jannik Vestegaard, 23, wa Werder Bremen, lakini beki huyo anasema hana habari (Daily Express).

CCM Yawatupa Nje Mawaziri Watatu, Majimbo Tisa Yapata Majibu
Mancini Aeleza Kwa Nini Amemuacha Kovacic Mateo