Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji kupitia Sera, Sheria na Taratibu kumewezesha kuongezeka kwa pato la taifa kutoka trilioni 39.9 mwaka 2021 hadi trilioni 45.2 mwaka 2022.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Juni 9, 2023 wakati akifungua Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara – TNBC, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu- Magogoni.

Amesema, TNBC itaendelea kuwa moja ya vyombo rasmi vya kuishauri Serikali kuhusu hatua muhimu za kuimarisha biashara kwa lengo la kujenga uchumi shirikishi.

Rais Samia pia ameihimiza TNBC, kufanya mashauriano ambam yataimarisha uwezo wa sekta binafsi nchini kuzalisha bidhaa za huduma zitak punguza uagizaji na kuongeza mauzo katika masoko ya kikanda na kimataifa na kusema amesema hatua hiyo itaiwezesha Tanzania kupunguza matumizi ya fedha za kigeni, kuongeza mapato na hivyo kuimarisha uchumi wa nchi.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amewaagiza viongozi katika ngazi zote kuendeleza majadiliano kupitia Mabaraza ya Biashara ya ngazi za mikoa na wilaya ili kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji.
Hali kadhalika, Rais Samia amesema Serikali inaendeela kuweka mkazo katika kutekeleza miradi ya kimkakati ikiwemo ya miundombinu, nishati na TEHAMA ambayo inawezesha kukua kwa biashara.

Kilio cha akina mama: GGML yagawa vitanda Nyankumbu
Rais Dkt. Mwinyi ashikiri Mkutano wa TNBC