Daktari wa Ikulu ya Marekani, Sean Conley amesema, Rais wa nchi hiyo Donald Trump hayumo tena katika kitisho cha kuweza kuambukiza virusi vya Corona. 

Taarifa hiyo ya uchunguzi wa kitabibu imetolewa katika kipindi ambacho rais Trump anajiandaa kuanzisha upya mikusanyiko ya kampeni na matukio mengine. 

Daktari huyo amesema Trump ametimiza vigezo vya usalama vya Vituo vya Udhibiti na Kinga kwa hivyo hatazamwi katika hatari ya kueneza maambukizi. 

Hata hivyo taarifa hiyo haijasema iwapo kiongozi huyo amepimwa na kuonekana hana virusi hivyo.

Wiki iliyopita Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter alitoa taarifa kuwa yeye na mkewe wamebainika kuwa na Corona ambapo alipelekwa hospitalini alikoruhusiwa kutoka siku tatu baadaye.

Watu 18 wauawa kwenye mapambano kati ya koo mbili
CUF Mtwara mjini wafungiwa kampeni siku 10