Rais wa Marekani anayeondoka madarakani, Donald Trump amesema hatahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya Joe Biden tarehe 20, Januari 2021.

Trump amesema hayo wakati ambapo taarifa za vyombo vya habari nchini Marekani zimeashiria uwezekano wa Rais huyo kukabiliwa na mashtaka kwa mara ya pili juu ya kumuondoa madarakani baada ya wafuasi wake kulivamia Bunge na kufanya fujo.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter Trump amesema kuwa, hatakwenda kwenye hafla ya kuapishwa kwa Joe Biden.

Uamuzi huo wa Trump unaleta ukakasi kutokana na kauli aliyotoa hapo awali juu ya kuhakikisha mchakato wa kukabidhi madaraka kwa amani.

Hata hivyo Rais mteule Biden amesema uamuzi huo wa Trump ni jambo zuri kwake.

Vyuo vya elimu ya juu vyatakiwa kusimamia maadili
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 9, 2021

Comments

comments