Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Sigmar Gabriel ameionya Marekani juu ya hatari ya kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv na kuupeleka Jerusalem akisema hatua hiyo haitapunguza mgogoro uliopo.

Sigmar Gabriel ametoa onyo hilo baada ya Rais Trump kusema atauhamisha ubalozi huo na kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas amesema kuwa hatua hiyo itasababisha madhara katika ukanda huo na dunia kwa ujumla.

Aidha, licha ya hatua hiyo kupingwa na Jumuiya ya kimataifa, Ikulu ya Marekani-White House imesema kuwa Rais Trump anatarajia kutoa tamko kuhusu suala hilo.

Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya rais wa Paletina, Nabil Abu Rudeineh, amesema kuwa Rais Abbas ameonya juu ya madhara yatakayotokea iwapo hatua hiyo itatekelezwa kutokana na hali halisi inayohusiana na mchakato wa kutafuta amani, usalama na uthabiti katika ukanda huo.

Chadema: Njaa na usaliti vinawafanya wahame
Video mpya ya Diamond Platinumz ''Sikomi''