Timu ya Taifa ya Ureno imefanikiwa kuibuka mabingwa wa soka Ulaya mwaka huu (Euro 2016) baada ya kuwachapa wenyeji Ufaransa 1-0 dakika chache zilizopita.

Éderzito António Macedo Lopes maarufu kama Eder ndiye aliyefanikiwa kupeleka kilio Ufaransa katika dakika ya 109,  baada ya kufumania nyavu umbali wa mita takribani 25.

Eder

Ulikuwa mchuano mkali uliolazimisha timu hizo kwenda zaidi ya dakika 90 za kawaida baada ya kubanana mbavu bila kumpata mbabe katika muda huo.

Ingawa Ureno walianza mechi kwa kuchechemea ndani ya dakika za mwanzo na kumpoteza nahodha wake Cristiano Ronaldo aliyelazimika kukaa nje ya chaki baada ya kupata majeraha, wameweza kufanya mabadiliko yaliyozaa matunda na kuandika historia ya kishujaa katika mashindano ya kombe la Ulaya (Euro 2016).

Ufaransa walimiliki zaidi mpira kwa asilimia 52 dhidi ya asilimia 48 ya Ureno.

Mbowe awazuia BAVICHA kwenda Dodoma, aandaa mbinu mpya
Makala: Marufuku ya mikutano ya hadhara haiathiri ‘nguvu ya Lowassa’