Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umetangaza kufanya maandamano nchi nzima Agosti 31 mwaka huu, ikiwa ni siku moja tu kabla ya tarehe iliyotangazwa na Chadema kufanya maandamano na mikutano nchi nzima.

Taarifa ya maandamano ya UVCCM imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka. Shaka amesema kuwa lengo la maandamano hayo ni kumpongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya tangu alipoingia madarakani.

Amesema kuwa tofauti na maandamano ya vyama vingine, maandamano yao ya amani na kwamba tayari wameshatoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi kama taratibu zinavyowataka.

Kauli ya UVCCM imekuja wakati ambapo bado kuna joto la chadema kutangaza kufanya maandamano na mikutano nchi nzima kwa kile walichodai kufanya operesheni ya kupinga ukandamizwaji wa demokrasia nchini waliyoipa jina la UKUTA na tayari Jeshil la Polisi limeshazuia kufanyika kwa maandamano kama hayo.

Dawasco Kanda Ya Tabata Yaendelea Kutoa Vifaa Kwa Wateja wake
Picha: Ziara ya Waziri Mkuu Inyonga, Milele