Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umemvaa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye sasa ni kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

UVCCM wamemtaka Sumaye kuacha mara moja kumkosoa Rais John Magufuli kwani hana sifa za kufanya hivyo kwa kuwa alishindwa kufikia hata theluthi ya kiwango cha utendaji kinachoonekana hivi sasa.

Hayo yalisemwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM ngazi ya Taifa, Shaka Hamdu alipokuwa akizungumza na wananchama wa chama hicho mkoani Kilimanjaro.

Alisema kuwa Sumaye na wanasiasa wengine  wanaokosoa utendaji wa Rais Magufuli ni wanasiasa mufilisi na kwamba wanatafuta umaarufu na kusikika kupitia jina la Rais Magufuli.

Aliwataka kutombugudhi Rais Magufuli kwa maneno yao na badala yake wakae kimya wamuache afanye kazi.

Mbali na Sumaye, Wanasiasa wengine waliowahi kumkosoa Rais Magufuli na kuonywa na UVCCM ni pamoja aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Edward Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

How To Write A Thesis In A Custom Essay
Kipre Tchetche Kuwavaa Wekundu Wa Msimbazi Jumapili