Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amesema kuwa hakuna mtu wa kumng’oa Iringa mjini kwani amejidhatiti vya kutosha.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam mara baada kufanyika kwa hafla ya uzinduzi wa kitabu cha sera ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)

Amesema kuwa hamahama ya madiwani wa chama hicho haiwezi kumyumbisha na kwamba chama hicho kimekuwa imara zaidi.

“Kuhama kwa madiwani hakuniyumbishi hata kidogo, mimi ni mwiba bungeni, mwiba ndani chama, kwa hiyo ni lazima mtu anituhumu tu, na namshangaa huyu Hapi anafanyakazi kwa mihemko, nadhani atapoa tu,”amesema Msigwa

 

Bill Cosby afungwa jela hadi miaka 10 kwa unyanyasaji kingono
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 26, 2018