Mkuu wa Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Tano Mwera amewataka wananchi wa wilaya na mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika ziara ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli inayofanyika kwa siku tatu mkoani humo.

Ameyasema hayo wilayani Busega Mkoani Simiyu alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa ziara hiyo ni fursa kubwa wananchi hao.

“Niwatake na kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika ziara ya rais Dkt. ambayo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo,”amesema DC Mwera

 

Video: Mkurugenzi Lutengano ataja mambo manne wilayani Magu
Amir Khan kusuka au kunyolewa leo, amuota Manny Pacquiao