Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kuhakikisha unawaondoa watu wote wanaoishi katika maeneo ya hifadhi na ushoroba wa wanyama wa Lyamgoroka.
Majaliwa ametoa aagizo wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Majalila wilayani Tanganyika.
“Hakikisheni mnatunza mazingira. Msiache wakate miti hovyo kwa sababu wanakausha vyanzo vya maji na kusababisha eneo kuwa hatarini kukumbwa na ukame, hivyo ni vyema wakaondolewa mapema,