Idadi ya vifo vilivyotokea baada ya tetemeko la ardhi lililotukia nchini Uturuki na Syria, imeripotiwa kufikia zaidi ya watu 16,000 huku watu 62,937 wakijeruhiwa.
Vifo hivyo, vilitokea baada ya maelfu ya majengo kuporomoka kutokana na tetemeko hilo la ardhi, huku Makundi ya waokoaji kutoka zaidi ya nchi 12 yakijiunga na maafisa wa Uturuki wa kukabiliana na hali za dharura katika juhudi hizo za uokoaji.
Maelfu ya watu wanaaminika kupoteza makazi yao na katika jimbo la Antakya waliokuwa wakaazi wa jengo lililoporomoka, walikusanyika nje katika moto waliowasha usiku kucha hapo jana wakiwa wamejifunika mablanketi kujaribu kujikinga kutokana na baridi kali.
Maeneo yaliyokumbwa na tetemeko hilo kubwa la ardhi ni oamoja na Mikoa ya Gaziantep, Osmaniye na Kilis wakati ambapo shutuma zinaendelea kutolewa dhidi ya serikali kutokana na kasi ndogo ya kushughulikia janga hilo.