Tangu Mwaka 1974, Dunia imekuwa ikiadhimisha Siku ya Mazingira kila Juni 5 ili kuhamasisha Serikali, Mashirika ya Biashara na Wananchi kushughulikia masuala nyeti yanayoathiri Mazingira.

Siku ya Mazingira ni jukwaa la Kimataifa la kuleta mabadiliko chanya kuhimiza watu kutafakari kuhusu kile wanachokula kutoka kwa Mashirika ya Biashara, kubuni mifumo isiyochafua mazingira kwa wakulima na kampuni za uzalishaji kuzalisha kwa njia endelevu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika fukwe za Coco (Coco beach), mmoja wa wadau wa mazingira aliyeshiriki kufanya usafi katika fukwe hizo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya HUDEFO, Sara Pima amesema kuwa wao kama watu wa mazingira wamejikita zaidi katika kutoa elimu ya mazingira katika jamii lengo ikiwa ni kuelimisha umuhimu wa kuhifadhi, kutunza mazingira.

Aidha kwa pamoja wadau hao wa mazingira wameiomba serikali kuboresha zidi mifumo ya mazingira ikiwemo mfumo wa utoaji adhabu kwa wanaochafua mazingira kwa kukusudia lakini pia mfumo wa ikolojia katika utunzaji.

Tanzania, msumbiji zajadili hali ya usalama
Ummy awataka waajiri kutowabana wafanyakazi