Taasisi ya Saratani Ohama iliyopo nchini Marekani inayomilikiwa na familia ya Dr Luke imekabidhi kiasi cha Us dollar 100,000 sawa na Tsh mil. 22 za kitanzania katika Hospitali ya Rufaa KCMC Mkoa wa Kilimanjaro kwaajili ya kuanza ujenzi wa hosteli za wagonjwa wa saratani.

Mkurugenzi mtendaji wa KCMC Dk.Gileard Masenga amesema kuwa hostel hizo zitawasaidia kwa kiasi kikubwa wagonjwa wenye kipato cha chini kwa gharama nafuu na wasiojiweza kusaidiwa bure.

Aidha ujenzi wa hosteli hizo utagharimu dola za kimarekani 250,000 zitakuwa na vitanda kati ya 45-65.

“Mwakajana nilikutana na familia ya Dr. Luke ambapo tulizungumza mambo mbalimbali na alitembelea sekta yetu ya saratani, aliahidi ataungana nasi katika kukamilisha wazo ambalo sisi tulikuwa tukilidhamilia la ujenzi wa hostel kwaajili ya wagonjwa wa saratani”amesema Dk Masenga

Mtaliano apewa nafasi kubwa Young Africans
TMDA: yafungua mashauri 146 makosa ukiukwaji wa Sheria