Watu wanne waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutungua helkopta na kusababisha kifo cha rubani, George Gower ambaye ni raia wa Uingereza, katika hifadhi ya akiba ya pori la Maswa wilayani Meatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 15 kila mmoja  jela (Jumla ya miaka 60) baada ya kukutwa na hatia.

Mahakama ya ya Wilaya ya Bariadi imewahukumu kifungo hicho Februari 11 mwaka huu baada ya kuwakuta na hatia katika makosa manne kati ya makosa kumi na moja yaliyokuwa yakiwakabili. Makosa hayo ni pamoja na kukutwa na bunduki mbili aina ya Riffle 303 na 458 pamoja na risasi sita kinyume cha sheria.

Kesi hiyo ilisomwa mara ya kwanza mahakamani hapo Februari 10 mwaka huu na watuhumiwa walirudishwa rumande hadi Februari 12 walipohukumiwa kifungo hicho baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha vielelezo vyao na watu hao kukiri makosa yao.

 

Akisoma hukumu hiyo, hakimu mkazi wa wilaya, Mary Mliyo aliwataja watu hao na umri wao kama inavyoonekana kwenye mabano kuwa ni Mange Buluma (47), Shija Mjika (38), Dotto Pangali (41) na Njile Gunga (28).

Sherehe za 'Valentine's Day' Zapigwa marufuku
Mwigulu Nchemba afanya ziara ya kushtukiza saa 7 usiku