Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ameweka wazi msimamo wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kuwashughulikia wasanii ambao wanavaa vibaya na kutumia lugha chafu kwenye kazi zao za sanaa.

Juliana Shonza amezungumza hayo ofisini kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe na kusema alipoteuliwa tu aliona kuwa kwenye sanaa hususani wasanii wamekuwa wakivaa vibaya kwenye kazi zao na kutumia maneno yasiyo na maadili.

‘Nilipoteuliwa tu ni jambo ambalo nilianza nalo ni mmomonyoka wa maadili kwa kweli imekuwa ni changamoto kubwa sana nimeshuhudia saizi hata ukiangalia kwenye nyimbo na kazi za sanaa lugha ambayo inatumika inakuwa siyo nzuri, lakini kama haitoshi kuna nyimbo ambazo zinaibwa ukifuatilia ndani unakuta maadili siyo mazuri’ amesema Shonza.

Ameongezea katika suala la mavazi na kusema kuwa yupo tayari kuliweka swala hilo wazi hasa kwa wasanii wa kike wajitahidi kuvaa vizuri.

“Hatuwezi kuacha hivi vitu vikawa vinaendelea tu kila taifa na misingi yake na tamaduni zake” Amesema Shonza.

Kutokana na tabia hiyo ameona kuna ulazima mkubwa wa Serikai kuingilia kati na kudhibiti tabia hizo.

Amesema lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha sanaa inakuwa katika misingi na maadili yanayofaa kwani kizazi cha watoto wa sasa kinawaangalia sana na kuiga mengi kutoka kwao.

Mbali na hilo Naibu Waziri wa Habari amesisitiza kuwa ni jukumu la viongozi kuhakikisha utamaduni wetu unaendelezwa na kusimamia misingi ya taifa.

 

Wolper aupa kiki wimbo wa Harmonize 'Shulala'
Daraja la Momba kuongeza kasi ya uzalishaji