Msanii wa filamu za Bongo, Wastara Juma amerejea nchini toka India alipokuwa ameenda baada ya kupata fedha alizochangiwa na Rais, John Pombe Magufuli na wananchi za kumsaidia kupata matibabu ya mguu na mgongo ambavyo vilikuwa vinamsumbua kwa muda mrefu.

Wastara amefanya mahojiano na vyombo vya habari mara tu baada ya kurejea nchini ambapo ametoa ripoti fupi kuhusiana na yaliyojiri huko India alipokuwa akifanyiwa matibabu.

Ameeleza kuwa amefanyiwa vipimo vyote na kugundulika kuwa ana tatizo kwenye fuvu la kichwa ambalo limeonekana kuwa na mpasuko kwa nje na kumsababishia uvimbe hali ambayo ilikuwa ikimpelekea kukosa usingizi. .

“Ni tatizo ambalo lilikuwa linahitajika kuchukuliwa umakini kwa sababu muda mwingi nilikuwa nalalamika kukosa usingizi, kitu ambacho mimi mwanzo nilikuwa nadhani labda ni kutokana na mawazo niliyokuwa nayo lakini siyo hivyo. Kwenye fuvu la kichwa kuna mpasuko kwa nje na kusababisha kama uvimbe jambo ambalo lilikuwa linanisababishia kukosa usingizi”, amesema Wastara.

Aidha kwa upande wa tatizo lake la miguu Wastara ameeleza kuwa unaendelea vizuri.

“Nimefanikiwa kupata dawa pia na ninatakiwa nitumie kila baada ya miezi mitatu na kama kuna uwezekano wa kupata matibabu hapa hapa nchini itakuwa vizuri. Wenyewe wamenishauri kama itawezekana niweze kupata bima ya afya kubwa kwa sababu kama kuna ulazima wa kurudi kila baada ya miezi mitatu iwe rahisi ili niweze kuangalia tatizo la kichwa kwa sababu sio jambo la kulifanyia masihara”.

Wastara amemalizia hivyo

 

Stamina: Basata na Wizara mnakuza au mnauwa sanaa?
Video: Ripoti yafichua mazito, CCM yaeleza siri ya Chadema kuitoa jasho Mbeya mjini