Jeshi la Polisi nchini Afrika Kusini, linawashikilia watu watatu wanaoripotiwa kuhusika na mauaji ya Rapper Kiernan Forbes, maarufu kama AKA na mara bada ya taratibu kukamilika wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka.
Chanzo kilicho karibu na uchunguzi wa mauaji ya rapper huyo, kimesema washukiwa hao walikamatwa na Polisi jijini Cape Town siku ya Jumapili Machi 26, 2023 baada ya kuwafuatilia kwa wiki nzima.
Msemaji wa Polisi wa Western Cape, Kanali André Traut, alipotafutwa ili kutoa maoni yake, alielekeza maswali hayo yapelekwe kwa ofisi ya Polisi iliyohusika kuwakamatwa iliyopo eneo la KwaZulu-Natal.
“Ni kesi ya KZN, tukipata taarifa, itapelekwa kwao. Unapaswa kuwasiliana nao kwa taarifasitaweza kuthibitisha iwapo watu hao walikamatwa mjini Cape Town na hata hivyo sidhani kama Msemaji wa polisi wa KZN, Kanali Robert Netshiunda pia atathibitisha kukamatwa kwa watu ha,” alisema.
AKA na rafiki yake Tebello ‘Tibz’ Motsoane, waliuawa kwa kupigwa risasi Februari katika Barabara ya Florida mjini Durban wakati Rapa huyo akiwa amesimama nje ya mkahawa wa Wish wakati mtu mwenye Bunduki alipomwendea na kumpiga risasi kichwani.