Hatimaye wachezaji Cristiano Ronaldo, Neymar na Lionel Messi wamefanikiwa kutinga kwenye orodha ya tatu bora ya wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa dunia maarufu kama Ballon d’or.

Messi na Neymar wanakipiga katika klabu ya Barcelona wakati Ronaldo anakipiga Real Madrid.

Huo ni mchujo wa mwisho kutoka katika majina 23 ya awali.

Sherehe zenyewe za kusaka mwanandinga bora wa dunia zitafanyika mwakani Januari 11.

Kwa sasa tuzo hiyo inashikiliwa na Cristiano Ronaldo.

Hafla ya kutangaza majina hayo imefanyika hivi punde nchini Uswisi.

Angalia Pogba Alivyoonyesha Kuguswa Na Shambulio La Paris
Kinachoendelea Ethiopia Chawakuna Azam FC