Klabu ya Arsenal ipo katika hatua nzuri ya kukamilisha mpango wa kuwasainisha mikataba mipya wachezaji wake Alexis Sanchez na Mesut Ozil chini ya ushawishi mkubwa unaoendelea kufanywa na meneja Arsene Wenger.

Taarifa zinasema kuwa, Wenger amependekeza wawili hao wasainishwe mkataba wa miaka miwili, ambayo itakua chachu ya kuanza kulipwa mishahara minono kutokana na kazi nzuri na kubwa wanayoifanya kwa ajili ya maendeleo ya Arsenal tangu walipotua klabuni hapo.

Mwishoni mwa juma lililopita Wenger aliwaeleza waandishi wa habari “Tupo tayari kuvunja benki kwa ajili ya kukamilisha mpango wa kusainiwa kwa mkataba mpya wa Ozil ambao utamuwezesha kupokea mshahara wa Pauni 250,000 kwa juma.”

Hali kadhali kauli kama hiyo aliitoa alipoulizwa kuhusu maendeleo ya mazungumzo kati ya uongozi wa Arsenal na Sanchez.

Wenger kwa sasa anamalizia muda wa mwaka mmoja uliosalia kwenye mkataba wake, lakini amekua na matumaini makubwa ya kuwabakisha wachezaji hao klabuni hapo kwa ajili ya maslahi ya baadae.

Kuhusu mchezo wa usiku wa kumkia hii leo Wenger, alisema kikosi chake kilionyesha ukomavu wa hali ya juu kufuatia soka safi ambalo limesaidia kupata ushindi mnono wa mabao sita kwa sifuri.

“Kijiamini kwa wachezaji wangu kulileta umakini na upinzani mkubwa dhidi ya Ludogorets, na jambo hilo linatuweka vizuri kuelekea katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili.

“Ni mapema kuzungumza matarajio makubwa tuliojiwekea, lakini naamni kwa kasi hii tutafanikiwa kufika mbali na ikiwezekana kufanya tunachokikusudia. Kwa sasa tuna kikosi kizuri na kinachojua namna ya kupambana wakati wote, lakini hatuna budi kuchukua tahadhari dhidi ya wapinzani wetu kila tunapokutana nao, kwa sababu lolote linaweza kutokea japo lengo letu ni kuhakikisha tunafanya vyema.” Alisema Wenger

The Gunners wamekua na mwanzo mzuri kwa msimu huu, kufuatia kushinda katika michezo saba iliyopita sambamba na ushindi mnono wa mabao sita kwa sifuri walioupata usiku wa kumakia hii leo dhidi ua Ludogorets kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mavugo Arejeshwa Kikosi Cha Kwanza
Video: Barcelona ilivyoiua Man City ya Guardiola