Mahakama Kuu ya Kanda ya Mwanza, leo imetoa uamuzi wa kesi ya kupinga ubunge Stanslaus Mabula (CCM) wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema, Ezekiel Wenje.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Jaji wa Mahakama hiyo leo ametupilia mbali madai ya Wenje na kubariki ushindi wa Mabula.

Wenje aliyekuwa mbunge wa Nyamagana awamu iliyopita, alifungua kesi namba 5/2015 akipinga matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaliyompa ushindi Mabula.

Katika mchakato wa kesi hiyo, Jaji Kakusulo Sambo, alikataa ombi la Wenje kutumia fomu ya Tume ya Uchaguzi namba 21B yenye matokeo ya vituo vyote 693 vya jimbo hilo kama ushahidi wa kesi yake.

Stanslaus Mabula akifurahia ushindi

Stanslaus Mabula akifurahia ushindi

Wafuasi wa CCM wakifurahia ushindi

Wafuasi wa CCM wakifurahia ushindi

Nape ashusha rungu kwa uongozi wa Yanga
Azam FC, Young Africans Zapata Baraka Za TFF