Alieyekuwa kiungo mahiri wa FC Barcelona Xavi amemshawishi kocha wake wa zamani Pep Guardiola kurudi klabuni.

Guardiola alifurahia maisha yenye mafanikio akiwa na klabu hiyo yenye maskani yake Camp Nou, kabla ya kuachana nao mwaka 2012, na kuelekea kunako klabu ya Bayern ambapo mkataba wake utamalizika msimu ujao, huku kukiwa na tetesi kuwa yuko mbioni kurejea Barcelona.

“Nilifurahia kipindi kizuri na chenye mafanikio wakati nilipokuwa na Pep pale Barcelona na naamini kwamba atafanya maamuzi sahihi siku moja ili kurudi tena Barcelona”, Xavi, ambaye kwa sasa yupo katika klabu ya Al Sadd, alikaririwa na tovuti ya klabu hiyo.

Joto Urais FIFA : Prince Ali Ampinga Platini
BASATA Yamfungia Shilole Kutojihusisha Na Muziki Mwaka Mmoja