Gwiji wa FC Barcelona, Xavi Hernández amelitoa la moyoni ambalo amedumu nalo kwa zaidi ya miaka mitano katika utendaji wake wa kazi yake ya soka uwanjani.

Xavi anayesukuma soka huko falme za kiarabu kwa sasa, amesema huenda angekua sehemu ya wachezaji wa FC Bayern Munich katika maisha yake ya soka kutokana na uongozi wa klabu hiyo kuwahi kuonyesha nia ya kutaka kumsajili wakati akiwa Camp Nou.

Xavi, amesema ofa hiyo aliipokea kwa mikono miwili na aliamini angebadilisha mazingira ya soka lake ambayo kwa kipindi kirefu yalituama nchini Hispania, lakini aliposaka ushauri kwa meneja wa Barcelona kwa kipindi hicho Pep Guardiola alishindwa kufanya maamuzi.

Amesema, Guardiola alimkatalia kuondoka FC Barcelona kwa maslahi ya klabu hiyo, na bila ajizi alikubaliana na maamuzi hayo kwa kuona kulikua na umuhimu wa mchango wake kuendelea kutumika.

Uamuazi wa Bayern Munich wa kutaka kumsajili Xavi, ulipitishwa mara baada ya fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2008 ambapo Hispania walifanikiwa kutwaa ubingwa wa barani humo kwa kuifunga Ujerumani kwenye mchezo wa hatua ya fainali.

Katika fainali hizo, Xavi alionyesha kiwango cha hali ya juu, na alikua msaada mkubwa kwa timu ya taifa ya Hispania ambayo ifanikiwa kushinda michezo yote sita na kutwaa ubingwa.

Katika mwaka huo Xavi alitangazwa kuwa mchezaji bora wa fainali za barani Ulaya, kitendo ambacho kiliongeza chachu kwa viongozi wa Bayern Munich kutamani kuwa nae kikosini mwao.

Xavi aliondoka FC Barcelona mwishoni mwa msimu uliopita na alijiunga na klabu ya Al-Sadd inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Qatar.

Hitzfeld Abariki Maamuzi Ya The Bavarians
Scholes Akibeza Kikosi cha Man Utd