Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwani michezo ya Ligi kuu bara bado ipo ambapo wamepanga kurekebisha makosa ambayo yamejitokeza katika mchezo dhidi Ruvu Shooting.

Akizungumza na moja ya chombo cha habari hapa nchini, Zahera ameshangazwa na mashabiki wanaolaumu kuhusu kupoteza mchezo wa kwanza na kusahau kwamba kuna michezo mingine kwenye ligi hiyo.

“Mpaka sasa nimeshajua makosa yalipo kwa wachezaji mbali na uchovu ambao ulituponza bado tuna michezo mingi mkononi hivyo tutafanya vizuri na kupata pointi tatu muhimu,”amesema Zahera

“Ligi haina mchezo mmoja tukasema imemalizika hapana bado muda wa kufanyia kazi makosa upo na tutafanya vizuri michezo mingine ambayo imebaki ni suala la kusubiri tu,” amesisitiza

Msimu huu Zahera amevunja rekodi aliyoweka msimu uliopita kwa kufungwa baada ya mchezo wa kwanza tofauti na msimu uliopita ambapo alipoteza baada ya kucheza michezo 19 amebakiwa na michezo 37 kufuta makosa yake.

Kampuni ya MTN yafunga huduma zake Nigeria
LIVE: Yanayojiri Bungeni jijini Dodoma