Hatimaye Rais John Magufuli amewapa wafanyakazi neema waliyokuwa wakiililia katika awamu zote za serikali zilizopita, baada ya kupunguza kodi ya mshahara kuwa katika kiwango cha tarakimu moja kwa asilimia.

hicho kilikuwa kilio kikubwa cha wafanyakazi nchini waliokuwa wakieleza kuzidiwa na mzigo wa kodi ya kipato cha mshahara wao, wakiitaka Serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza asilimia za makato hayo kuwa kutoka tarakimu mbili kuwa tarakimu moja.

Akitoa hotuba yake kwa wafanyakazi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi, Rais Magufuli alitangaza kushusha kiwango cha tozo la kodi kwenye mshahara (PAYE) kutoka asilimia 11 hadi asilimia 9.

Aidha, Rais Magufuli aliwataka wafanyakazi hao kuendelea kuvumilia kwa kutokuwepo kwa ongezeko la mshahara kwani hivi sasa anaendelea na jitihada za kukuza uchumi na kubana mianya ya rushwa nchini. Pia, aliwataka waajiri wote nchini kuhakikisha wanatoa mikataba kwa wafanyakazi wao.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alieleza kuwa zoezi la kuwabaini watumishi hewa limebaini upotevu wa shilling bilioni 11.6 kwa mwezi ambazo ni sawa na shilingi bilioni 139 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa kwa watumishi hewa 10,295.

Wabunge wa CCM wapinga kwa sauti Bunge kuoneshwa Live, Ukawa waja na mbinu mbadala
Video: Davido aonekana akimpiga ‘shabiki’ kama mwizi