Mahakama Kuu nchini Kenya imeamua kwamba wanandoa wanaoachana hawatagawana mali nusu kwa nusu kama ilivyokuwa awali, bali kila mmoja atatakiwa kuchukua mali yake kwa kuonesha vithibitisho.

Mbele ya jopo la majaji watano, likiongozwa Naibu Jaji Mkuu Philomema Mwilu ilielezwa kuwa kila mwanandoa, atatakiwa kuthibitisha mchango wake au mali zilizopatikana kitu kitakachorahisisha mgawanyo wa mali.

Maajaji wa Mahakama ya Juu nchini Kenya. Picha ya

Uamuzi huo, unafanyika kwa mujibu wa marekebisho ya Ibara ya 45 (3), ya Usawa katika Ndoa huku ukiweka bayana kila mwanandoa kutakiwa kuonesha mchango wake kwenye mali zilizopatikana.

Aidha, Mahakama ilielezwa kuwa usawa kwenye ndoa haimaamishi uwepo wa nusu kwa nusu ya umiliki wa mali baada ya ndoa hiyo kuvunjika, na kwamba mgawanyo unapaswa kutolewa kwa kuangalia mchango binafsi wa kila mmoja.

Mpango awataka Wanazuoni kuipaisha Tanzania uandishi wa Vitabu
Kasi ufugaji wa Samaki yaongezeka nchini