Mwanaume mmoja, Kelvin Muthom (28), amefariki dunia baada ya kuzama Mto Nyamindi uliopo Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya, wakati akisherehekea kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa (birthday), akiwa na mkewe.

Muthom ambaye alikuwa mfanyakazi wa Hoteli katika Mji wa Kimbimbi, aliteleza akiwa juu ya mwamba karibu na mtu huo na kuzama wakati mkewe na rafiki aliokuwa nao wakishuhudia.

Rafiki wa marehemu, George Macharia ambaye ni mkaazi wa Kaunti ya Meru ameviambia vyombo vya habari kuwa marehemu aliomba kazini mapumziko ya siku moja, ili apate nafasi ya kusherehekea kumbukizi ya siku yake hiyo.

“Wanakijiji walisaidia kutoa kutoa taarifa kwa mkuu wa polisi wa eneo na baadaye kuwaeleza ndugu za marehemu,” alisema Macharia wakati akiongea na Citizen TV.

Mkuu wa Polisi Msaidizi wa eneo la Ngucui, George Mungai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema marehemu alizama mtoni majira ya saa kumi jioni, Februari 2, 2023 na hadi leo mwili wake bado haujapatikana.

“sote tunafahamu historia  ya mto huu, ingawa sio msimu wa mvua tunapaswa kuchukua tahadhari kubwa. Tunaendelea kuutafuta mwili wa marehemu, tunaamini leo tunaweza kuupata baada ya kutofanikiwa jana,” aliongeza.

Serikali kufanya marekebisho gridi ya taifa
Samsung Electronics East Africa yazindua toleo jipya la Simu