Hali ya afya ya Spika mstaafu, Samuel Sitta si nzuri,baada ya Serikali kumpeleka nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi.

Habari za uhakika  zinasema Sitta alipelekwa Ujerumani juzi kwa matibabu baada ya afya yake kubadilika ghafla.

“Nilimtembelea siku moja kabla ya kupelekwa nje ya nchi, kwa kweli hali ya afya yake ilikuwa imedhoofu, namwombea Mungu amsaidia apone haraka ili arudi kuendelea na majukumu yake.

“Nimesikitishwa mno na taarifa za kuzushiwa kifo mzee wangu huyu, Mungu ni mwema najua bado anampigania uhai wake…hii tabia ya mitandao ya kijamii kumzushia mtu kifo sijui inafaidika nini.

“Mpaka anaondoka nchini kwenda matibabu natambua amekuwa asikumbuliwa mno na tatizo la miguu, sasa mimi si daktari wake siwezi kuongeza zaidi,”kilisema chanzo chetu.

Septemba 19, mwaka huu, Rais Dk. John Magufuli alimtembelea Sitta hospitalini alikolazwa kwa muda sasa kumjulia hali, kisha kumwombea dua Mungu amsaidie.

Siku iliyofuata Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa naye alimtembelea hospitalini kumjulia hali.

Sitta ameshika  nyadhifa mbalimbali, zikiwamo za Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, uwaziri na ubunge kwa kipindi kirefu.

Picha 8: Rais Magufuli azindua rasmi ndege mbili mpya za Air Tanzania
Yaya Toure Awahurumia Wabaguzi Wa Rangi