WATU 12 wamepoteza maisha na wengine 28 kujeruhiwa katika ajali ya basi mali ya Kampuni ya New Force lenye namba za usajili T426 DEU iliyotokea mkoani Njombe.

Akizungumza na Habarileo Mtandaoni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Prudenciana Protas amesema majeruhi 16 kati ya 28 wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa na waliobaki wanaendelea na matibabu katika Hospitali za mikoa ya Ruvuma na Njombe.

“Majeruhi walikuwa 28 lakini waliobaki katika hospitali hizi mbili hadi sasa ni majeruhi 12 watatu wakiwa Ruvuma Hospitali na wengine tisa wakiwa hapa Njombe lakini kati ya hao waliopo Njombe wanne hali zao ni mbaya,” alisema Kamanda Protas.

Kamanda huyo wa Polisi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa Dereva wa basi hilo, Charles Kirwa ambaye basi lilimshinda na kupinduka hivyo kusababisha vifo hivyo 12 na majeruhi 28.

 

Balaa la mabilioni ya Escrow lamuibua tena Kafulila
Young Africans Watofautiana Na TFF

Comments

comments