Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Nickson Simon ‘Nikk wa Pili’ amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kanda ya Kijiografia wa Shirika la Direct Aid, Tariq Fahim wa Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo Kuwait.

Katika mazungumzo yao, DC Simon amemueleza Mkurugenzi huyo juu ya kampeni yake ya Kisarawe yenye ujuzi, ambapo Tariq Fahim amesema wamepanga kujenga Chuo kikubwa cha Ufundi katika Tarafa ya Chole, ili kusaidia ajenda ya Mkuu wa Wilaya hiyo ya Kisarawe yenye ujuzi.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Kisarawe, Nickson Simon pia amepokea msaada wa mitambo 200 ya Solar kwa ajili ya wananchi wa Kitongoji cha Mlegele utakaowasaidia kuondokana na tatizo giza.

Mbali na kugawa solar hizo Mkurugenzi huyo pia amezindua Mashine ya kusaga kata ya Manerumango, ameshuhudia pia ujenzi wa kisima kirefu cha shule ya Sekondari Gongoni, Ghala la Chakula Manerumango na Miradi ya Ufugaji.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi huyo aliambatana na Mkurugenzi wa kanda kusini mwa Afrika, Mukhtaar Sayyid, Mkurugenzi Mkuu Tanzania Dkt. Adam Osman na Makamu Mkurugenzi Mkuu Tanzania Mohamed Orabi.

Album mpya ya Barnaba 'yaanika' siri za Diamond
Watawa Kanisa Katoliki watekwa nyara na wasiojulikana