Baada ya kuwa katika matibabu nchini Kenya kwa kipindi kirefu kufuatia kupigwa risasi, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa mara ya kwanza ameweka ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter unaosomeka ”Mungu ni Mwema”

Hapo jana Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo ‘Chadema’ Freeman Mbowe alitoa taarifa rasmi za maendeleo ya afya yaTundu Lissu akisema anaendelea vizuri na ametolewa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU na sasa afya yake imehimarika.

Hii ndio Tweet ya kwanza ya Lissu

Mbowe alisema watu wataanza kuona picha za Lissu kwa mara ya kwanza akiwa hospitali na kuskia sauti yake kwa mara ya kwanza tangu alipopelekwa jijini Nairobi kwa ajili ya matibabu.

Aluta.jpegLisu.jpeg

 

Video: ACT- Wazalendo wazungumzia mwanachama wao kujiengua
Mfalme wa Oman aunga mkono juhudi za JPM