Siku chache baada ya Rais John Magufuli kumuondoa Mama Anne Kilango Malecela katika nafasi ya Ukuu wa Mkoa, mwanasiasa huyo machachari ameelezea hali ya moyo wake.

Ni dhahiri kuwa wengi wanaajaribu kupata picha ya namna alivyolipokea suala hilo wakijaribu kukumbuka kauli za kishujaa za mwanzo za Mama Malecela baada ya kupata uteuzi huo mwezi mmoja uliopita.

Pamoja na hayo, Mama Malecela ameliambia gazeti la The Citizen kuwa amelipokea suala hilo kwa moyo mweupe.

“Nimeupokea uamuzi wa Rais kwa moyo mweupe. Hilo ndilo ninaloweza kusema hivi sasa,” Mama Malecela anakaririwa.

Katika hatua nyingine, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Alphonce Gagambobyaki alisema kuwa ofisi yake haifahamu mtu aliyempa Mkuu wa Mkoa ripoti aliyoitumia kutoa maelezo kuwa hakukuwa na watumishi hewa mkoani humo.

 

MARY MAJALIWA ATOA MSAADA KWA AKINA MAMA WALIOJIFUNGUA
Jonjo Shelvey: Sitaisaliti Newcastle Utd Hata Ikishuka Daraja