Meneja mpya wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte ametenga kiasi cha Pauni milioni 57, kwa lengo la kuwahamisha wachezaji wawili kutoka nchini Italia, Antonio Candreva pamoja na Leonardo Bonucci.

Conte ambaye kwa sasa anamalizia mkataba wa kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Italia kinachoshiriki fainali za mataifa ya barani Ulaya (Euro 2016) huko nchini Ufaransa, amedhamiria kufanya usajili huo ikiwa ni sehemu ya sera yake ya kutaka kuirejeshea heshima Chelsea FC.

Mshambuliaji wa pembeni Candreva, mwenye umri wa miaka 29, ameripotiwa kuwa tayari kuihama klabu yake ya sasa ya SS Lazio na malengo yake ni kutaka kucheza soka nchini Italia akiwa na klabu ya Inter Milan, lakini Conte anatarajia kuutumia mwanya huo ili kumshawishi acheze soka nchini England.

Antonio Candreva

Thamani ya Candreva, imeshatajwa kuwa ni Pauni milioni 25.

Kwa upande wa beki wa kati wa klabu ya Inter Milan, Leonardo Bonucci, huenda kukawa na ugumu kwa Chelsea kukamilisha usajili wake, kutokana na uwepo wa mkataba wa miaka mitatu unaombana mchezaji huyo.

Leonardo Bonucci

Hata hivyo Antonio Conte anaamini kuna haja kwa viongozi wa The Blues kuongeza nguvu za kumshawishi wakala wa Bonucci pamoja na upande wa klabu ya Inter Milan ili biashara hiyo iweze kukamilishwa kwa wakati.

Kwa kuona umuhimu wa jambo hilo, sehemu ya fedha iliyotengwa kwa ajili ya usajili wa wachezaji hao wawili wa Italia, kiasi cha Pauni million 32 huenda kikatumika kwa ajili ya ushawishi wa kumuhamisha Bonucci.

Bonucci, mwenye umri wa miaka 29, anapigiwa upatu wa kusajiliwa na klabu ya Chelsea chini ya utawala wa Antonio Conte, kutokana na safu ya ulinzi ya The Blues kuwa na mapungufu, kufuatia kuumia kwa Kurt Zouma.

Mikel Arteta Kumsaidia Pep Guardiola Man City
Aman Vincent: Malinzi Anahusika Katika Mgogoro Wa Stand Utd