Mshambuliaji Olivier Giroud usiku wa Jumatano ameibuka shujaa baada ya kufunga mabao yote matatu, Arsenal ikishinda 3-0 ugenini dhidi ya wenyeji Olympiakos katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Georgios Karaiskakis, Giroud alifunga mabao hayo dakika za 29, 49 na 67 kwa penalti na kuifanya The Gunners kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi hilo kwa kufikisha pointi tisa, nyuma ya Bayern Munich iliyomaliza na pointi 15.

Lakini Arsenal inafuzu hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa kwa wastani wa mabao tu, kwani imefungana kwa pointi na Olympiakos iliyoishia nafasi ya tatu.

Mchezo mwingine wa kundi hilo, Bayern Munich imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Dinamo Zagreb, mabao yote akifunga Robert Lewandowski dakika ya 61 na 64 Uwanja wa Maksimir.

Chelsea nayo imekuwa timu ya tatu ya England kwenda 16 Bora ya michuano hiyo baada ya Manchester City na Arsenal, kufuatia ushindi wa mabao 2-0  dhidi ya FC Porto Uwanja wa Stamford Bridge katika mchezo wa Kundi G.

Ivan Marcano Sierra alijifunga dakika ya 12 kuipatia The Blues bao la kwanza kabla ya Willian Borges Da Silva kufunga la pili dakika ya 52.

Mchezo mwingine wa kudi hilo, Dynamo Kyiv imeshinda 1-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv, bao pekee la Denys Garmash dakika ya 16 Uwanja wa Olimpiki.

Chelsea inamaliza kileleni mwa kundi hilo kwa pointi zake 13, ikifuatiwa Kyiv pointi 11, Porto pointi 10 na Maccabi ambayo haina pointi.

Katika mchezo wa Kundi E, Barcelona imelazimishwa sare ya 1-1 na Bayer 04 Leverkusen iliyoanza kupata bao kupitia kwa Javier Hernandez ‘Chicharito’ dakika ya 23, kabla ya  Lionel Messi kuwasawazishia mabingwa hao watetezi dakika ya 20 Uwanja wa BayArena.

Mchezo mwingine wa kundi hilo, Roma imetoka 0-0 na BATE Borisov Uwanja wa Olimpico.

Barca inamaliza kileleni kwa pointi zake 14, ikifuatiwa na Roma pointi sita na sawa na Bayer 04 Leverkusen, wakati imeshika mkia kwa pointi zake tano.

Valencia CF imefungwa 2-0 nyumbani na Lyon ua Ufaransa katika mchezo wa Kundi H.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mestalla, mabao ya wageni yamefungwa na Maxwell Cornet dakika ya 37 Alexandre Lacazette dakika ya 76.

Mchezo mwingine wa kundi hilo, KAA Gent imeshinda 2-1 dhidi ya Zenit St Petersburg mabao yake yakifungwa na Laurent Depoitre dakika ya 18 na Danijel Milicevic dakika ya 78, huku la wageni likifungwa na Artem Dzyuba dakika ya 65 Uwanja wa Ghelamco Arena.

Timu zilizofuzu 16 Bora ni Real Madrid, Paris Saint-Germain, VfL Wolfsburg, PSV, Atletico Madrid, Benfica, Manchester City, Juventus, Barcelona, Roma, FC Bayern Munich, Arsenal, Chelsea, Dynamo Kyiv, Zenit St Petersburg na KAA Gent.

Zilizopenya 16 Bora UEFA Champions League 2015-16
Hussein Machozi: Nimeacha Muziki rasmi