Mbunge wa Kawe na Askofu wa Kanisa Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekiri kupokea barua ya wito wa kuitwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Barua ya ofisi ya Bunge iliyomtaka Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima na mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa kwenda mbele ya kamati ya Bunge Agosti 23 na 24.

“Nimepokea barua ya Spika kwenda kwenye kamati, nitakwenda. Nimesema hapa kwa kuwa aliyenitumia barua ameweka mitandaoni akisema kwanini nimesema hapa na yeye aniambie kwa nini aliweka mitandaoni,” amesema Gwajima

Askofu Gwajima amesema atakwenda kwenye kamati hiyo na atasimamia ukweli kama ambavyo imani yake inamtuma.

 “Nitakwenda kwenye kamati wategemee ukweli nitasema ukweli kwa kuwa imani ya CCM ni ukweli na nitaongeza mengine ambayo sijawahi kusema. Lazima tusimamie nchi na watoto wa watoto wetu,” amesema askofu Gwajima

Young Africans yasitisha kambi Morocco
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 23, 2021