Hii inahusu tukio lililotokea hivi karibuni katika eneo la Namanga jijini Dar es Salaam baada ya Mke wa waziri (jina limehifadhiwa) kumtunishia misuli askari wa usalama barabarani.

Askari huyo aliyetajwa kwa jina la Koplo Deogratius Mbango, alimkamata dereva wa mama huyo baada ya kuvunja sheria kwa kusimama kwenye alama za pundamilia ambazo ni maalum kwa wapiti njia, hata hivyo mama huyo alimtaka akari huyo kukaa pembeni akiweka mbele jina na cheo cha mmewe. Kwa mujibu wa askari huyo mama huyo alimtusi kwa kumuita ‘mshenzi asiye na akili’.

Ndipo askari huyo alipompigia simu kamanda wa Polisi kikosi cha usalama barabarani wa Kinondoni na maongezi yakarekodiwa.

Ijumaa, Rais Magufuli aliagiza askari huyo kupandishwa cheo kwa kusimamia sheria.

Zinedine Zidane Ajipa Matumaini Kwa Cristiano Ronaldo
Claudio Ranieri: Nitakua Wa Mwisho Kufahamu Matokeo