Mshambuliaji kutoka nchini Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo yu shakani kucheza mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Man City utakaounguruma mjini Madrid usiku wa jumatano.

Ronaldo alikosa mchezo wa ligi ya nchini Hispania uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita ambapo Real Madrid walipambana na Real Sociedad na kuambulia ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Mshambuliaji huyo ameripotiwa kuwa katika hali ya 50 kwa 50 kutokana na vipimo alivyofanyiwa jana asubuhi, licha ya kuonekana akifanya mazoezi  mepesi pembezoni mwa wachezaji wenzake.

Meneja wa kikosi cha Real Madrid, Zinedine Zidane ameonyesha kuwa na matumaini makubwa ya kumtumia Ronaldo katika mchezo huo ambao utakua na umuhimu mkubwa kwake pamoja na kwa klabu hiyo kongwe kwa ujumla.

Amesema mshambuliaji huyo hali yake imeanza kuridhisha na hana shaka na harakati za kumtumia katika mchezo dhidi ya Man City.

Ronaldo hakujumuishwa katika kikosi cha Real Madrid kilichocheza mchezo wa mkondo wa kwanza juma lililopita dhidi ya Man City kufuatia maumivu wa nyama za paja, na alitarajiwa huenda angecheza mwishoni mwa juma kwenye mchezo wa ligi lakini haikuwa hivyo.

Hata hivyo indaiwa kwamba Ronaldo anapata shinikizo kubwa la kuepuka kucheza kwa sasa, kutoka kwa daktari wa timu ya taifa ya Ureno, Nuno Campos, ambaye anahofia huenda akaongeza tatizo ambalo litamsababishia kuzikosa fainali za mataifa ya barani Ulaya (Euro 2016) ambazo zitaanza kuunguruma mwezi ujao nchini Ufaransa.

Wakati huo huo mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa, Karim Benzema naye yupo shakani kucheza mchezo wa jumatano dhidi ya Man City, kufuatia maumivu wa goti yanayomkabili kwa sasa.

Wenger Asalimu Amri Kwa Mashabiki Wanaompinga
Audio: Sikiliza ‘vutankuvute’ kati ya 'trafiki' na Mke wa Waziri iliyomfikia Rais Magufuli