Australia imedukuliwa habari za siri kuhusu mpango wake wa kijeshi wa serikali uliokuwa ukihusu ndege mpya ya kijeshi na manowari zilizokuwa katika matengenezo.

Takriban GB 30 za data zimedukuliwa zilizokuwa na mkandarasi mmoja aliyekuwa akihusika katika utengenezaji wa ndege hiyo na manowari mpya ya kijeshi ya jeshi la nchi hiyo iliyokuwa inatarajiwa kuanza kazi hivi karibuni.

Aidha, maafisa usalama wa mitandaoni nchini Australia walimtaja mdukuzi wa nyaraka hizo kuwa anajulikana kwa  jina ‘Alf’ baada ya jina la muigizaji wa kipindi cha runinga nchini humo cha ‘Home and Away kuonekana.

Hata hivyo, kwa mujibu wa maafisa usalama wa nchi hiyo, wamesema kuwa Udukuzi wa nyaraka hizo ulianza mwezi Julai mwaka uliopita lakini idara ya usalama nchini Australia haijkujua chochote hadi mwezi Novemba.

Video: Eminem amchana Trump
Mkubwa Fella alimfanya Aslay awe na wasiwasi

Comments

comments