Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amewasilisha ombi la kisheria la kutaka ripoti ambayo inaweza kusababisha kushtakiwa kwake kwa tuhuma za ubadhilifu na kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu kubatilishwa.

Kwa mujibu wa msemaji wa Rais, Vincent Mangwenya amesema nyaraka hizo zimewasilishwa katika Mahakama ya Kikatiba na kusema rais ametaka ripoti hiyo ifanyiwe mapitio, na itangazwe kuwa batili na ipuuzwe.

Shamba lililoteta tafrani baada ya kuibiwa kwa pesa zinazomuweka Rais Ramaphosa ‘kitanzini’. Picha ya Mail & Guardian.

Kupitia andiko lake lenye kurasa 59, Ramaphosa anataka mchakato wowote wa kumshtaki uzuiwe, akisema “hatua zozote zinazochukuliwa na Bunge kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kinyume cha sheria na ni batili.

Asema, “Wabunge wa Afrika Kusini leo hii wanatarajiwa kujadili ripoti iliyowasilishwa juma lililopita na timu maalumu ya uchunguzi kuhusu madai Ramaphosa kuficha wizi mkubwa wa pesa katika shamba lake nchini humo.”

Maporomoko yasababisha vifo watu 27
Young Africans yaitangazia vita Namungo FC