Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Amanda Hawkins amekamatwa kwa tuhuma za mauaji ya wanae wawili, aliowaacha na kuwafungia kwenye gari lenye joto kwa muda wa saa 15.

Jeshi la polisi la Texas nchini Marekani anapoishi mwanamke huyo limeeleza kuwa watoto hao mmoja akiwa na umri wa mwaka mmoja tu na mwingine miaka miwili waliachwa kwenye gari usiku kucha wakilia na kwamba mama yake alikuwa akiendelea na starehe umbali mrefu akiwa na rafiki yake.

Watoto hao waliokuwa kwenye hali mbaya, walifariki saa chache baada ya kukimbizwa hospitalini baada ya kutolewa kwenye gari siku iliyofuata.

“Hili ni tukio baya zaidi, la kusikitisha na la uzembe uliosababisha mauaji nililowahi kulishuhudia kwa miaka 37 ya utumishi wangu ndani ya jeshi hili,” amesema mkuu wa polisi wa eneo la Kerr, kupitia taarifa yake kwa umma.

Tamko hilo linaeleza kuwa wakati watoto hao wakiendelea kulia, kuna mfanyakazi wa eneo hilo alimfikishia taarifa mama yao aliyekuwa anakula bata, lakini alipuuzia.

Ripoti ya pili mchanga wa madini yaiva, kukabidhiwa kwa JPM
Video: Rungwe azungumzia uteuzi wa Anna Mghwira, aeleza maamuzi yake kama akipata uteuzi