Kikosi cha Azam FC leo  mchana kilipofanya mazoezi ya viungo ndani ya bwawa la kuogelea kwenye Hoteli ya Mtoni Marine, ilipofikia timu hiyo Visiwani hapa.

Programu hiyo ilisimamiwa na Kocha Msaidizi wa Viungo wa Azam FC, Borges Pablo, ambapo aliweza kuwafanyisha mazoezi tofauti wachezaji ndani ya maji, ambayo walifurahishwa nayo.

Mazoezi hayo ni ya kuwaweka sawa wachezaji kabla ya mchezo wa kwanza wa kirafiki visiwani hapa dhidi ya Kombaini ya Wilaya Mjini itakayofanyika leo saa 2.30 Usiku.

Rais Wa Besiktas Atamani Kumsajili Balotelli
Video Mpya: Kala Jeremiah Ft Miriam Chirwa – Wanandoto