Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amesema mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Dkt. John Pombe Magufuli hataongeza muda madarakani baada ya kumaliza vipindi viwili.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni unaofanyika leo wilayani Chato, mkoani Geita  Dkt. Bashiru amesema kuwa kuna watu wanaodai endapo CCM itapata wabunge wengi watabadili katiba ili Magufuli aendelee kubaki madarakani hata pale atakapomaliza muda wake. Amesema watu hao wamefilisika kisiasa.

“Nitumie jukwaa hili ambalo wewe unazaliwa kukanusha kidogo uvumi kwamba CCM inataka kushinda viti vingi vya ubunge ili tubadilishe katiba uongezewe  wewe muda, tumekanusha mara nyingi lakini watu waliochoka na kufirisika kisiasa wanaendelea kutuchokonoa, ameshasema naomba pia nisisitize anaomba miaka yake mitano ikamilike kumi na hataongeza hata sekunde,” amesema Dkt. Bashiru.

Aidha, Dkt. Bashiru amesema kuwa baada ya CCM kumaliza mzunguko wa kwanza wa kampeni zake  kitafanya mizunguko mingine ili kufikia maeneo mengi zaidi.

Mgombea wa chama hicho, leo septemba 14, 2020 anaendelea na kampeni wilayani Chato mkoani  Geita.

Bares: Dodoma Jiji FC walituzidi
Vandenbroeck atuma salamu Biashara Utd Mara