Klabu ya Olympique Lyon imesisitiza kuwa tayari kumuachia mshambuliaji wao kutoka nchini Ufaransa Alexandre Lacazette, ili ajiunge na Arsenal ya England endapo watapokea ofa itakayoendana na thamani yake.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo ya mjini Lyon nchini Ufaransa, imeeleza kuwa, Arsenal itawalazimu kutoa kiasi cha Pauni milioni 40 kama kweli wanamuhitaji Lacazette.

Jana klabu hiyo ilithibitisha kupokea ofa ya The Gunners na kuiweka kapuni iliyokua na thamani ya Euro milion 35 sawa na Pauni milioni 29.3.

Klabu ya West Ham Utd iliwahi kujaribu kutuma ofa ya Pauni milioni 32 kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, lakini hawakufanikiwa kumpata kwa kigezo cha ofa hiyo kuwa ndogo.

Video: CHADEMA watoa tamko kufanya mikutano nchi nzima tarehe 1 september 2016
Rais Wa Besiktas Atamani Kumsajili Balotelli