Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji aliyekuwa ametekwa na watu wasiojulikana amepatikana akiwa hai jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Kamishna Lazaro Mambosasa amesema kuwa Mo Dewji amepatikana kuamkia usiku wa leo majira ya saa tisa usiku.

“Tunashukuru Mungu tumempata Mo Dewji usiku wa kuamkia leo, majira ya saa nane kwenda saa tisa, tulipata taarifa kuwa Mo Dewji amepatikana, ikabidi tufike nyumbani kwake, kujiridhisha kwake, kweli tumempata na kuongea naye ni mzima,”amesema Mambosasa

Kwa upande wake, Mohamed Dewji amewashukuru Watanzania wote kwa maombi yao ambayo yamemuwezesha kupatikana akiwa salama.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 20, 2018
Jiwe la Kg 37 alilopigwa mwanafunzi aliyebakwa latua mahakamani

Comments

comments